Tuzo hiyo ni mara ya kwanza kutolewa ndani ya Yanga mara tu baada ya kuingia mkataba wa miaka mitatu na Kampuni ya Bima ya Taifa (NIC) ambao wameweka sh. milioni 900
Kiungo mshambuliaji wa Yanga, Stephan Aziz KI, ameshinda Tuzo ya Mchezaji Bora wa Oktoba ndani ya timu yake.
Aziz Ki ameshinda tuzo hiyo akiwazidi Max Nzengeli na Dickson Job ambao aliingia nao Tatu Bora.
Tuzo hiyo ni mara ya kwanza kutolewa ndani ya Yanga mara tu baada ya kuingia mkataba na Kampuni ya Bima ya Taifa (NIC) ambao wameweka sh. milioni 900 kudhamini tuzo hiyo kwa miaka mitatu.
16:30 - 29.10.2023
Ligi Kuu: MO Dewji ateua wajumbe 21 Baraza la Ushauri la Simba SC
Dewji amesema katika kipindi cha miaka mitano iliyopita tangu waanze safari ya mabadililko ya klabu yao, wamepiga hatua kubwa.
Mbali na tuzo lakini Aziz Ki anatarajiwa kupokea kiasi cha fedha taslimu sh. milioni 4 ikiwa ni zawadi ya mshindi kwa kila mwezi.
Mwezi Oktoba ulikuwa ni mzuri kwa Aziz Ki ambaye aliisaidia timu yake kupata ushindi kwenye michezo mitatu kati ya minne walioshuka dimbani huku yeye akifunga mabao manne.
Kumbuka ndani ya Oktoba ni kiwango chake alichoonesha wakati Yanga wakiwaburuza Azam kwa mabao 3-2 huku Aziz Ki akifunga mabao yote matatu 'Hat trick'.
13:07 - 30.10.2023
KANDANDA Robertinho sasa aigeukia Yanga Jumapili
Robertinho amesema mchezo wa 'derby' siku zote huwa ni mgumu na ndio maana anahitaji muda kwa ajili ya kukiandaa kikosi chake ili kufanya vizuri kwenye mchezo huo.
Kwa upande wa Max, ndani ya Oktoba yeye amefunga mabao matatu huku Job ambaye ni mlinzi wa kati hakufunga bao lolote.
Tuzo hizo huamuliwa na mashabiki ambao hupewa fursa ya kupiga kura kupitia App za Yanga na matokeo yake hutangazwa baada ya mwezi kukamilika.