Gamondi akuna kichwa makundi Afrika

© Kwa Hisani

KANDANDA Gamondi akuna kichwa makundi Afrika

Zahoro Mlanzi • 12:28 - 12.10.2023

Tayari Yanga wameshatambua kundi ambalo watakuwa kupambania pointi likiwa ni pamoja na Al Ahly ya Misri kwenye kundi hilo.

Kocha Mkuu wa timu ya Yanga SC, Miguel Gamondi, ameweka wazi baada ya kutinga hatua ya makundi kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika, wana kazi kubwa ya kufanya.

Tayari Yanga wameshatambua kundi ambalo watakuwa kupambania pointi likiwa ni pamoja na Al Ahly ya Misri kwenye kundi hilo.

Timu zingine ni Medeama ya Ghana na CR Belouizdad ya Algeria.

Yanga ilikuvunja rekodi ya kufuzu hatua hiyo baada ya miaka 25 kutokana na ushindi dhidi Al Merrikh ya Sudan kwa jumla ya mabao 3-0 ambapo katika mchezo wa kwanza uliopigwa Rwanda, Yanga iliibuka na ushindi wa mabao 2-0 ule wa nyumbani walishinda bao 1-0.

Akizungumza na Pulsesports, Gamondi amesema amefurahishwa na kiwango kizuri kilichoonyeshwa na wachezaji wao na kufanikiwa kutinga hatua hiyo lakini amewapa angalizo la kuhakikisha wanajipanga mapema kuweza kufanya makubwa kwenye hatua hiyo.

“Sasa ni muda wa kuangalia mechi zilizopo mbele yetu, tunafanya maandalizi hatua kwa hatua mechi kwa mechi, kabla ya kufikiria hatua inayofuata ya michuano ya kimataifa.

“Najua ukubwa na ugumu wa makundi ya Ligi ya Mabingwa kwa sababu zinashiriki timu bora sasa lazima kila mchezaji anatambua nini ambacho tunahitaji kufanya ili tuweze kufanya vizuri kwa sababu hatuwezi kubweteka kwa kuwa tayari tumeshafika katika hatua hii maana nguvu na mikakati inatakiwa kuanzia sasa kwenda mbele,” amesema Gamondi.