Katika mchezo huo, Al Ahly ndio walikuwa wa kwanza kupata bao kupitia kwa Reda Slim aliyefunga dakika za majeruhi kabla ya mapumziko.
Kocha wa Klabu ya Al Ahly, Marcel Koller, amemtupia lawama mwamuzi Beida Dahane kwa madai ya kushindwa kuwapa mkwaju wa penalti kwenye mechi ya ufunguzi ya michuano ya AFL dhidi ya Simba ambapo mchezo huo ulipigwa Uwanja Mkapa, Dar es Salaam na kumalizika kwa sare ya 2-2.
Akizungumza na vyombo vya habari, Koller ambaye timu yake ilipata sare hiyo baada ya kusawazisha kipindi cha pili kupitia kwa Mahmoud Kahraba, amesema katika kipindi cha kwanza licha ya kuwa walicheza vizuri na kupoteza nafasi za kufunga lakini walistahili penalti ambayo mwamuzi wa kati raia wa Mauritania alikataa.
21:50 - 20.10.2023
FOOTBALL Simba SC, Ahly zafungana 2-2 michuano ya AFL
Wekundu wa Msimbazi walipoteza nafasi ya kupata ushindi katika robo fainali ya kwanza baada ya kutoka sare 2-2 na Al Ahly na watalazimika kushinda nchini Misri ili kufuzu nusu fainali
"Timu yangu ilikuwa bora kwenye kipindi cha kwanza, tulitengeneza nafasi za kufunga hatukuzitumia na baadaye tukanyimwa penalti ambayo kwa upande wangu naona ilistahili tuipate, sijui kwanini mwamuzi ameikataa licha ya kuangalia kwenye VAR," amesema.
Katika mchezo huo, Al Ahly ndio walikuwa wa kwanza kupata bao kupitia kwa Reda Slim aliyefunga dakika za majeruhi kabla ya mapumziko.
19:00 - 19.10.2023
KANDANDA Makocha Simba SC, Al Ahly wapigana mkwara
Kocha wa Simba SC, Robert Oliviera, na wa Al Ahly, Marcel Koller, wajiandaa kwa mchezo wa ufunguzi wa michuano ya AFL nchini Tanzania.
Hata hivyo mara baada ya kuanza kipindi cha pili Simba walisawazisha kupitia kwa Kibu Denis na kisha Sadio Kanoute kuongeza la pili kwenye dakika ya 57.
Matokeo ya sare ya 2-2 yanaiweka katika mazingira mazuri Al Ahly ambayo Jumanne watakuwa nyumbani kuwakaribisha Simba kwenye mechi ya marudiano na mshindi wa jumla atavuka kwenda hatua ya nusu fainali.
20:30 - 19.10.2023
FOOTBALL Simba defender ready to roar against African giants Al Ahly
Simba SC defender vows to play fearlessly against Al Ahly as the African Football League debuts in Dar es Salaam.
Wakati huohuo, kikosi cha Al Ahly, kimeondoka nchini Tanzania na kurudi kwao Misri kwa ajili ya kwenda kujiandaa na mchezo wa marudiano dhidi ya Simba mechi ambayo itachezwa Oktoba 24 kwenye Uwanja wa Kimataifa wa Cairo.