Sina presha yoyote tumejiandaa kama tunavyofanya kwenye mechi nyingine, kikubwa kesho ni kujiepusha na makosa kwani makosa madogo yanaweza kuamua mechi
Kocha wa Klabu ya soka ya Yanga, Miguel Gamondi, amesema hana presha kuelekea mchezo wa kesho dhidi ya Simba.
Gamondi amesema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam kuelekea mchezo huo ambao utapigwa Uwanja wa Mkapa, Dar es Salaam.
15:33 - 04.11.2023
Kariakoo Derby Robertinho: Mechi za 'derby' ndio zangu
Mimi ni raia wa Brazil ni nchi ya mpira, binafsi napenda kucheza mechi kubwa na kwa siku ya kesho nimekiandaa kikosi changu kwa ajili ya kucheza mchezo dhidi ya Yanga.
Kocha huyo raia wa Argentina, amesema maandalizi waliyofanya ni ya kawaida kama ambavyo huwa wanafanya kwenye mechi nyingine na kwamba kikubwa anachoamini mechi itakuwa nzuri kwa pande zote mbili.
Gamondi amesema muhimu katika mchezo wa kesho ni kuepuka kufanya makosa kwani kosa dogo linaweza kuamua mechi.
21:45 - 03.11.2023
Ligi Kuu Simba SC yakiri Yanga wagumu kufungika
Yanga wana wachezaji wengi wazuri lakini wao hawahofii mchezaji mmoja mmoja bali timu nzima.
"Sina presha yoyote tumejiandaa kama tunavyofanya kwenye mechi nyingine, kikubwa kesho ni kujiepusha na makosa kwani makosa madogo yanaweza kuamua mechi," amesema.
Aidha Gamondi alipoulizwa kuhusu rekodi ya Yanga kushindwa kupata ushindi dhidi ya kocha wa Simba, Robertinho kwa mechi kadhaa, amesema yeye hajawahi kufungwa na Simba kwani katika mechi ya Tanga walitoka sare hivyo amesema hana rekodi yoyote anayotakiwa kuivunja.
09:35 - 04.11.2023
Ligi Kuu Azizi Ki, Robertinho watwaa Tuzo ya Oktoba
Hiyo inakuwa ni tuzo ya pili kwa Azizi Ki ndani ya wiki hii ambapo hivi karibuni alishinda tuzo ya mchezaji bora ndani ya Yanga.
Mchezo wa kesho utachezeshwa na Mwamuzi Ahmed Arajiga kutoka Manyara kama ilivyotangazwa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF).