Baadhi ya nyota hao ni Opa Clement wa Besiktas ya Uturuki na Aisha Masaka wa BK Hancken ya Sweden.
Wachezaji watano wanaocheza timu mbalimbali barani Ulaya, Amerika na Asia, wameitwa katika kikosi cha timu ya Taifa ya Wanawake ya Tanzania 'Twiga Stars' kwa ajili ya mchezo wa kuwania kufuzu michuano ya Afrika kwa Wanawake (WAFCON) mwakani nchini Morocco.
Twiga Stars inatarajia kuumana na Togo katika raundi ya pili ya michuano hiyo, mchezo utakaopigwa Jumatano ijayo jijini Dar es Salaam.
18:30 - 17.11.2023
KANDANDA Aucho wa Yanga afungiwa mechi tatu Ligi Kuu
Khalid Aucho amefungiwa mechi hizo na faini ya shilingi Tsh500,000 kutokana na utovu wa nidhamu aliouonesha Novemba 8
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), timu hiyo itaingia kambini Novemba 22.
Taarifa hiyo imewataja nyota hao wanaocheza nje ya nchi kuwa ni beki Julieath Singano anayecheza Juarez ya Morocco, viungo Enekia Kasonga wa Eastern Flames ya Saudi Arabia na Diana Lucas wa Ameds FK ya Uturuki.
22:00 - 15.11.2023
KANDANDA Simba SC kutimua wachezaji wavivu, wasiojituma
Tumekubaliana kutoendelea kufanya kazi kwa mazoea na kwamba tutachukuwa hatua stahiki ili kuboresha kikosi chetu hasa katika usajili unaokuja wa Januari
Pia wapo washambuliaji, Opa Clement wa Besiktas ya Uturuki na Aisha Masaka wa BK Hancken ya Sweden.
Kikosi hicho cha Kocha, Bakari Shime, kinaundwa na wachezaji wengi nyota wa timu ya JKT Queens ambao ni mabingwa wa Ligi Kuu ya Wanawake na Bingwa wa Afrika Mashariki na Kati pamoja na wawili wa Simba Queens na mmoja wa Yanga Princess.
19:00 - 16.11.2023
Football Yanga SC yashika nafasi ya nne ubora Afrika
Mafanikio hayo yametokana na kushinda ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania, ubingwa wa FA Cup na kufika hatua ya fainali ya Kombe la Shirikisho barani Afrika.
Baada ya mchezo huo, utakaopigwa Uwanja wa Azam Complex, tiimu hizo zitarudiana mapema Desemba Uwanja wa Kegue jijini Lome na mshindi wa jumla atafuzu kwa fainali hizo.